Roma Mkatoliki na wenzake wapatikana.

Roma Mkatoliki na wenzake wapatikana salama.

Msanii Roma Mkatoliki na wenzake watatu wamepatikana leo waki hai baada ya kutoweka kwa kutekwa siku ya Jumatano wakiwa katika studio za Tongwe Records.

Baada ya taarifa ya Kamishna wa Polisi Kamanda Simon Sirro iliyotolewa leo asubuhi na kusema polisi wanaendelea na upelelezi, wasanii hao wote wamepatikana wakiwa hai na sasa wapo katika kituo cha polisi cha Oysterbay.

Mmiliki wa wa Tongwe Records J Murder amethibitisha wasanii wake hao kupatikana na sasa wapo kituo cha polisi wakitoa maelezo.
Mpaka wakati huu mke wa Roma Mkatoliki amefika kituoni hapa hapa na kuambiwa wasubiri nje utaratibu wa kipolisi uendelee kufanyika. 

Mbali na hilo mwanasiasa Julius Mtatiro ambaye naye alikwenda kituoni hapo ili kumuona rafiki yake Roma Mkatoliki kwa mamcho yake, amezuiliwa getini kuingia kituoni hapo.

"Hali ya hapa Oysterbay Polisi si nzuri. Polisi wamenizuia nje ya geti, wamenishauri nisikae eneo hili. Mimi sikuwa na nia mbaya, nilitaka kumuona Roma kwa macho yangu. And he is my good friend. Wito wangu ni kwa wanasheria wa Roma, hakikisheni mnawahi hapa, atoe maelezo kwa polisi nanyi mkiwepo. Hebu mambo haya tuyachukulie serious zaidi." ameandika Julius Mtatiro. 

0 comments: