Feature news

UPDATES: Roma mkatoliki na Wenzake wameondolewa Polisi Oysterbay na kupelekwa Mwananyamala Hospitali

Huyo ni wakili wa Roma akiongea muda huu na vyombo vya Habari.

Roma mkatoliki na Wenzake wameondolewa Polisi Osterbay na kupelekwa Mwananyamala Hospitali Kuangaliwa afya.

Habari kamili zitafuata
Learn more »

Roma Mkatoliki na wenzake wapatikana.

Roma Mkatoliki na wenzake wapatikana salama.

Msanii Roma Mkatoliki na wenzake watatu wamepatikana leo waki hai baada ya kutoweka kwa kutekwa siku ya Jumatano wakiwa katika studio za Tongwe Records.

Baada ya taarifa ya Kamishna wa Polisi Kamanda Simon Sirro iliyotolewa leo asubuhi na kusema polisi wanaendelea na upelelezi, wasanii hao wote wamepatikana wakiwa hai na sasa wapo katika kituo cha polisi cha Oysterbay.

Mmiliki wa wa Tongwe Records J Murder amethibitisha wasanii wake hao kupatikana na sasa wapo kituo cha polisi wakitoa maelezo.
Mpaka wakati huu mke wa Roma Mkatoliki amefika kituoni hapa hapa na kuambiwa wasubiri nje utaratibu wa kipolisi uendelee kufanyika. 

Mbali na hilo mwanasiasa Julius Mtatiro ambaye naye alikwenda kituoni hapo ili kumuona rafiki yake Roma Mkatoliki kwa mamcho yake, amezuiliwa getini kuingia kituoni hapo.

"Hali ya hapa Oysterbay Polisi si nzuri. Polisi wamenizuia nje ya geti, wamenishauri nisikae eneo hili. Mimi sikuwa na nia mbaya, nilitaka kumuona Roma kwa macho yangu. And he is my good friend. Wito wangu ni kwa wanasheria wa Roma, hakikisheni mnawahi hapa, atoe maelezo kwa polisi nanyi mkiwepo. Hebu mambo haya tuyachukulie serious zaidi." ameandika Julius Mtatiro. 
Learn more »

MRISHO MPOTO: Nilijua leo tungeambiwa Roma amepatikana


Mrisho Mpoto anasema alikwenda leo asubuhi na mapema akiwa na matarajio kuwa huenda polisi leo wangeweza kuwapa taarifa kuwa wasanii hao wamepatikana lakini kwa mujibu wa taarifa ya Kamishna Simon Sirro ni kwamba mpaka sasa wasanii hao hawajapatikana na hawafahamiki wapo wapi, ila amesema bado wanaendelea na upelelezi.

"Sisi kama wasanii tunaendelea kusikitishwa na kuumizwa na suala zima la Roma Mkatoliki na ndiyo maana nimekuja hapa asubuhi na mapema nilikuwa najua kwamba tutaambiwa Roma amepatikana yupo hapa salama na vitu kama hivyo, kwa hiyo matarajio na nilichokisikia vimetofautiana lakini siwezi kuingilia mamlaka," alisema Mrisho Mpoto 

Mbali na hilo Mrisho Mpoto ametoa wito kwa jamii 

"Wito wangu kwa jamii ni utulivu na kuendelea kumuomba Mungu na kuacha waandishi wa habari na vyombo husika viweze kufanya kazi zake" alisema Mrisho Mpoto 
Learn more »

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI LEO


Learn more »

MAREKANI YASHAMBULIA KWA MAKOMBORA KAMBI YA JESHI LA SYRIA


Marekani imefanya mashambulizi ya anga katika kambi ya jeshi la Syria katika kujibu mapigo ya tukio linalodaiwa kuwa shambulizi la silaha za kemikali dhidi ya raia katika mji unaoshikiliwa na waasi.Makombora 59 aina ya Tomahawk yamerushwa kutoka kwenye meli mbili za kijeshi kutoka bahari ya Mediterranean.Rais Donald Trump amesema wameshambulia kambi ya jeshi ya Shayrat ambayo ilifanya mashambulizi ya kemikali siku ya jumanne.
Hili ni shambulizi la kwanza la Marekani moja kwa moja dhidi ya serikali ya Syria. Urusi ambayo inamuunga mkono rais Bashar al-Assad, imeshutumu shambulizi hilo.
 
Kambi ya jeshi ya Shayrat inavyoonekana baada ya mashambulizi 
 
Meli ya jeshi la Marekani ikirusha makombora ya Tomahawk
Learn more »